Hakuwa wa kishua, nyumbani ni very poor sasa akasoma ili ile hali aje kuitoa Akapenda shule binti hakuleta masihala, kitabu akapiga kweli mpaka kayumba akajielewa Darasa aliongoza mapenzi hakuyatukuza anadai elimu kwanza, mapenzi yapo yatafuata. Akawa wa mfano, tangu yupo la tano hakupiga zogo, yeye ni busy na masomo akawapa moyo wazazi wasio na kipato Baba akazidi kutoa jasho ili binti afike chuo Mama alimpa pendo binti aliyependa masomo kazi za ndani ni mwiko hakupenda alete mchezo Kwa upendo wa wazazi binti aliongeza juhudi shule alipewa nafasi ili binti afike mbali ( yeah )
Alipenda sana mbeleni aje kuwa doctor au la ... kama ikibidi mwanasheria akaweka nia kwa kupania binti akazipiga mia wasiopenda wakachukia Kafika cha tatu binti hajamjua mvulana kawabwaga sana mpaka wote waka'surrender Akauacha usichana, changamoto zikamuandama mtoto wa kike akapambana shetani asipate mwanya Alipendwa sana wote walimwita shujaa kitaa akapata jina kwa tabia anazoonesha
yeah .... kosa moja
yeah ..... kosa moja
yeah
Mafataki wengi walitaka kumrubuni wote wakaishia mbavuni chup chup kifungoni Miaka haisimami akamaliza sekondari nyumbani akavuta pozi daily anasali asifeli ukafika wasaa tokeo likatangazwa binti amekikunja kijiti tena cha kwanza kwa furaha, baba na mama wakajichanga mwana akapata mazaga pongezi kwa alichofanya Masomo ya udokta watu wakamsihi sana shule asilete masihala dunia isije kucheka Akatoa ahadi kwa majirani wazazi na marafiki kwamba shule atakazana Akaanza cha tano kidato mambo yako sawa mabanda anapiga sana, binti hakutaka masihala kama kawa, wote waliomtokea walijutia chaga walichezea sana wote wakamwona anaringa Ni somo la ujana ndo lililoanza kumchanganya Teacher alidokeza jambo binti akataka kufanya Anadai tendo ni bora kuliko neno so, ni bora afanye tendo ili apevuke kwenye somo Akafanya tendo madai ni jaribio baada ya tendo binti akapata kilio Sio uchungu wa kiapo ndo unamfanya awe mdogo watu wameshtuka ana zigo, sio dogo miezi mitano Cha sita kidato binti akaachishwa masomo wote waliomuona yuko moto daily wanakosa maelezo Akazidiwa mama kwa ugonjwa wa moyo Baba akageuka kichaa wanadai msongo wa mawazo Dunia inacheka binti amepoteza imani kosa kafanya, anawaza amewapa nini wazazi